Home Kitaifa Striker Singida kavunja na kuweka rekodi ligi kuu

Striker Singida kavunja na kuweka rekodi ligi kuu

9553
0
SHARE

Mshambuliaji wa Singida United raia wa Rwanda Danny Usengimana amevunja rekodi ya cleen sheet ya golikipa wa Azam Razak Abarola.

Mbali na kuivuruga rekodi hiyo ya golikipa raia wa Ghana, Usengimana ameweka rekodi ya kufunga bao la kwanza ligi kuu Tanzania bara ukiwa ni msimu wake wa kwanza tangu aanze kucheza Tanzania akitokea kwao Rwanda.

Usengimana alimfunga Razak dakika ya 39 kipindi cha kwanza kuipa Singida United bao la kuongoza.

Golikipa wa Azam Razak Abarola amepoteza rekodi yake ya cleen sheet baafa ya kuruhu goli kwenye mchezo dhidi ya Singida United uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Kabla ya mchezo Razak alimudu kucheza mechi nne mfululizo bila kurusu bao (sawa na dakika 360). Ndanda 0-1 Azam, Azam 0-0 Simba, Azam 1-0 Kagera Sugar, Azam 1-0 Lipuli, ni mechi ambazo golikipa huyo alisimama langoni na kutoka salama.

Razak ndio alikuwa golikipa pekee ambaye hajaruhusu goli tangu kuanza kwa msimu kabla ya mechi ya jana. Kwa hiyo hakuna timu ambayo haijaruhusu bao hadi sasa.

Kinda wa Azam Peter Paul pia amejiwekea rekodi yake alipoisawazishia timu yake bao, Paul amefunga goli la kwanza tangu amejumuishwa kwenye kikosi cha wakubwa akitokea (Azam U20) huku ukiwa ni mchezo wake wa kwanza katika ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here