Home Kimataifa Atletico vs Chelsea: Simeone ataendeleza rekodi bora ya nyumbani?

Atletico vs Chelsea: Simeone ataendeleza rekodi bora ya nyumbani?

3842
0
SHARE

Atlético wamepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 23 waliyocheza chini ya Diego Simeone katika uwanja wa Vicente Calderón – leo wanacheza mchezo wao wa kwanza wa ulaya katika dimba lao jipya la Estadio Metropolitano, dhidi ya klabu ya Chelsea.

Swali kubwa katika lips za anayefuatilia mtanange huu, sio kuhusu Chelsea, ni je Rojiblancos na Diego Simeone wataweza kuendeleza walipoachia katika dimba la

Vicente Calderón, uwanja ambao ulikuwa ngome hasa kwenye michuano ya ulaya.

Rekodi za Atletico kwenye Michuano ya ulaya katika uwanja Vicente Calderón

Kiujumla: Mechi 142, Wameshinda 104, Sare 24 Wamepoteza mechi 14.

European Cup/UEFA Champions League: Wamecheza mechi 51, Wameshinda 36, sare 11 na wamepoteza mechi 4.

UEFA Cup Winners’ Cup: P29 W20 D6 L3

UEFA Cup/UEFA Europa League: P62 W48 D7 L7

Rekodi za kiujumla katika michuano ya ulaya zinavutia, lakini rekodi zao chini Diego Simeone zinavutia zaidi. Wamepoteza mchezo mmoja tu wa ulaya – kipigo vs Benfica miaka miwili iliyopita, mechi ya pili ya hatua ya makundi msimu wa 2015/16 – hii ndio mechi pekee aliyopoteza Simeone katik uwanja wa nyumbani katik kipindi cha miaka 6 ya uongozi wake na Atletico.

Rekodi za Atletico katika michuano ya ulaya chini ya Diego Simeone

Wamecheza mechi: 23

Wameshinda: 18

Sare: 4

Wamepoteza: 1

Wamefunga magoli: 43

Wamefungwa magoli: 6

Leo Jumatano wanakutana na vijana wa Conte, Chelsea ambao mchezo wa mwisho kukutana ilikuwa April 30 katika uwanja wa Stamford Bridge, The Blues akafa 1-3 nyumbani.

Kiujumla timu hizi zimeshakutana mara 5, Chelsea mara 1 tu, kafungwa mara 2 na sare 2.

:

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here