Home Kimataifa Barry avunja rekodi ya Ryan Giggs huku Lacazette akivunja rekodi iliyowekwa 1988

Barry avunja rekodi ya Ryan Giggs huku Lacazette akivunja rekodi iliyowekwa 1988

9265
0
SHARE

Mwaka 1998 ndipo Garreth Barry alianza kucheza soka la kulipwa na usiku wa leo tarehe 25 September Barry amecheza mchezo wake wa kulipwa wa 633 katika ligi kuu ya nchini Uingereza.

Barry hadi sasa ameichezea ligi kuu ya Uingereza kwa miaka 19 huku akiitumikia kwa dakika 52,871 na sasa anakuwa amempita Ryan Giggs ambaye alikuwa akishikilia rekodi kucheza michezo 632 ya ligi hiyo.

Pamoja na kuifikisha rekodi hiyo lakini Barry alishindwa kuikoa West Bromich Albion kupewa kipigo cha bao 2 kwa sifuri na Arsenal waliokuwa katika dimba lao la Emirates.

Kubwa lingine katika mchezo huo ni Alexandre Lacazzete ambaye amevunja rekodi iliyowekwa mwaka 1988 na Brian Marwood ya kufunga katika michezo yao mitatu ya mwanzo ya ligi ya Epl.

Lacazette huyo huyo aliipatia Arsenal bao lingine dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati huku hilo likiwa bao lake la 4 msimu huu idadi sawa na mabao waliyofunga West Brom hadi sasa.

Kwa matokeo hayo yanawafanya Arsenal kubaki katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama zao 10 huku Manchester City wakiwa kileleni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here