Home Ligi EPL Ubinafsi na kumtusi Ronaldo kulivyomuondoa Nistelrooy Man Utd

Ubinafsi na kumtusi Ronaldo kulivyomuondoa Nistelrooy Man Utd

9169
0
SHARE

Ruud van Nistelrooy aliuzwa kutoka Manchester United kwenda Santiago Bernabeu kutokana na Sir Alex Ferguson kuchoshwa na tabia zake.

Kwa mujibu makala zilizoabdijwa na mwandishi Alastair Campbell – aliyekuwa mkuu wa mawasiliano wa Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blaire, ambaye pia alikuwa na ukaribu na Mzee Fergie – ameandika kwamba kocha wa United alikuwa anachukizwa sana na tabia za Van Nistelrooy kabla ya kumuuza mwaka 2016.

Nistelrooy alikuwa mbinafsi sana mwenye kujisikia na Fergie hakuwa na namna ya kudili nae,” aliandika Campbell.

“Jambo la mwisho ambalo Fergie alishindwa kuvumilia ni pale alipomwambia Cristiano kwamba amepata baba mpya kwa Carlos Queiroz (msaidizi wa Ferguson), alimwambia maneno haya kipindi ambacho Ronaldo alitoka kumpoteza baba yake mzazi.

“Carlos Queiroz alijaribu kumwambia anatakiwa kuheshimu wenzio, bado Van Nistelrooy hakunali.

“Hata hivyo baadae aliomba radhi kwa CR7, lakini Ronaldo hakutaka hata kumsikia.

“Fergie aliposikia kuhusu jambo hilo alimuondoa Van Nistelrooy mazoezini na kumtaka arudi nyumbani.”

Van Nistelrooy hakukaa sana United baada ya tukio hilo na mwishoni mwa msimu aliuzwa kwenda Real Madrid na miaka 3 baadae akaungana na tena na Ronnie Santiago Bernabeu lakini kwa mara nyingine hakukaa sana akaondoka katikati ya msimu kwenda Hamburg.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here