Home Kimataifa Matokeo ya Carbao Cup, Bundesliga, Serie A na La Liga haya hapa

Matokeo ya Carbao Cup, Bundesliga, Serie A na La Liga haya hapa

5615
0
SHARE

Michy Batshuayi alifunga hat trick yake ya pili tangu aanze kucheza soka la kulipwa huku Kennedy na Cherly Musonda wakifunga kila mtu bao moja wakati Chelsea wakiitwanga Nottingam Forest mabao 5 kwa 1 huku la Forrest likifungwa na Tendayi Garikwa.

Marcus Rashford naye alifunga mabao mawili huku Jesse Lingard na Anthony Martial wakifunga bao moja moja wakati Manchester United wakiendeleza dozi ya mabao 4 dhidi ya Burton Albion, lakini Burton walipata bao moja kupitia kwa Lloyd Dyer.

Arsenal waliwapiga Doncaster Rovers bao 1 lililofungwa na Theo Walcott huku Everton wakiichapa Sunderland mabao 3 kwa 0 kupitia Calvert Lewin(2) na Bayr Oumar.

Manchester City waliipiga West Bromich Albion bao 2 kwa 1 huku mabao yote ya City yakifungwa na Leroy Sane na lile la Albion likifungwa na Claudio Yacob

Kule Serie A Ac Millan waliipiga SPAL 2013 mabao 2 kwa 0 huku mabao ya Milan yakiwekwa kimiani na Ricardo Rodriguez na Kessie, Juventus wakiwa ugenini waliipiga Fiorentina bao 1 kwa sifuri.

Napoli walikuwa ugenini dhidi ya Lazio ambapo Maria Callejon, Kalidou Koulibaly na Dries Mertenes waliipa ushindi Napoli wa bao 4 kwa 1 huku lile la Lazio likifungwa na Stefan De Vrij.

Bundesliga nako Pierre Aubbameyang ameendelea kutaka wakati Dortmund ikiwapiga Hamburger Sv bao 3 kwa 0 huku mengine yakifungwa na Shinji Kagawa na Christian Pulisic.

Bayern Leverkusen walikubali kupigwa bao 2 kwa 1 na Hertha Berlin, huku wanyonge uwanjani na wababe wa majukwaani Fc Cologne wakiendelea kucharazwa uwanjani baada ya kupigwa bao 1 kwa 0 na Frankfurt.

Kule Hispania hadi dakika 45 za mwanzo zinamalizika Real Madrid walikuwa wamebanwa mbavu na Real Betis ya bila bila huku Leganes mchezo wao na Girona ukiisha bila bila.

Athletico Madrid waliokuwa ugenini waliichapa Bilbao kwa mabao mawili kwa moja, mabao ya Madrid yakiwekwa kimiani na Yannick Carrasco na Angel Correa huku lile la Bilbao likifungwa na Raul Garcia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here