Home Kitaifa Ndondo Cup 2017 Makundi yamepangwa Mwanza

Ndondo Cup 2017 Makundi yamepangwa Mwanza

2757
0
SHARE

Historia inaandikwajijini Mwanza, kwa mara ya kwanza michuano ya Sports Extra Ndondo Cup itachezwa kwenye mji huu wa miamba. Tayari makundi yameshapangwa pamoja natimu zote kugawiwa vifaa kabla ya kuanza kwa mashindano.

Timu 16 ambazo zitashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza zimepangwa kwenye makundi manne ambapo kila kundi lina timu nne. Draw imechezeshwa usiku wa Jumatatu September 18, 2017 na iliruka Live kupitia kipindi cha Sports Bar cha Clouds TV.

Game ya ufunguzi itapigwa kati ya Buzuruga Terminal vs Nyegezi Terminal Jumatano ya September 20, 2017 kwenye uwanja wa Nyamagana. Unaambiwa timu hizi zina upinzani mkubwa katika jiji hili la Mwanza.

Tayari viingilio vimeshatangazwa ambapo mdau wa soka atatakiwa kulipia shilingi 2000 tu kushuhudia mechi moja ya Ndondo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here