Home Kitaifa Manara akanusha kukalia kuti kavu kwa Omog – Simba wakiifuata Mbao kesho

Manara akanusha kukalia kuti kavu kwa Omog – Simba wakiifuata Mbao kesho

5558
0
SHARE

Na Thomas Ng’itu

Klabu ya Simba kesho alfajiri itaondoka Jijini na ndege ya Air Tanzania kuelekea mkoani Mwanza kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao, utakaopigwa Alhamis CCM Kirumba.

Ofisa habari wa klabu hiyo Haji Manara alisema, klabu yao inaondoka mapema kwenda kujiandaa na mchezo huo,huku wakiwa na imani ya kupata pointi tatu baada ya msimu uliopita kusumbuliwa na klabu hiyo.

Timu itaondoka kesho alfajiri kwenda kujiandaa na mechi hiyo,kikosi kizima chote kitakuwepo huko wachezaji ambao tutawakosa ni Shomar Kapombe na Said Nduda ambao ni majeruhi lakini wengine wote watakuwepo katika kikosi,” Manara.

Akizungumzia taarifa zilizosambaa, kuhusu kocha wao Joseph Omog kupewa mechi tatu alisema hizo ni taarifa ambazo zimekuzwa na baadhi ya watu na sio uongozi wa klabu ya Simba.

Rais amekaa na mwalimu na kumwambia kuwa bado anahitajika katika kikosi hico, huku akimsisitizia kuwa hakupewa mechi zozote kama ambavyo inavyosambazwa hivyo Omog ataendelea kuwa kocha wetu,”.

Manara pia alihoji kuwa unawezaje kumfukuza kocha ambaye ameifanya timu kufunga mabao 10 katika mechi tatu, huku vilabu 15 vilivyobaki katika ligi vikiwa vimefunga mabao 9 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here