Home Kimataifa Baada ya matokeo mabovu, bosi wa zamani na mchezaji wa zamani wa...

Baada ya matokeo mabovu, bosi wa zamani na mchezaji wa zamani wa Arsenal watimuliwa Fc Wolfburg

6315
0
SHARE

Alama nne katika michezo minne ni kigezo tosha kwa Wolfburg kumtupia virago Adries Jonker, Wolfburg ambao msimu uliopita nao ulikuwa mgumu kwao wamechoshwa na kocha wao na kuamua kumtimua.

Katika kuonesha kwamba Wolfburg wanahitaji mabadiliko wameamua kumtimua na kocha msaidizi kwa klabu hiyo Uwe Speidel na makocha wengine waliokuwa katika benchi la ufundi akiwemo nguli wa zamani wa Arsenal Fredrick Ljunberg

Jonker alikuwa kocha katika academy ya klabu ya Arsenal 2014-2015 na mwezi February alipoachana na klabu hiyo ndipo alijiunga na Wolfburg na tangu kipindi hicho klabu hiyo imekuwa ikipata tabu kupata matokeo.

Wakati huo huo taarifa iliyotolewa hii leo na klabu hiyo imesema Martin Schdmit aliyekuwa akiifundisha klabu ya Mainz inayoshiriki ligi hiyo ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Wolfburg.

Martin Schdmit aliiongoza Mainz hadi ikashiriki michuano ya Europa msimu wa mwaka 2015/2016 na Wolfburg wamempa mkataba kocha huyo raia wa Uswisi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here