Home Uncategorized “Tumepoteza, tunajipanga kwa ajili ya Simba”-Ettiene

“Tumepoteza, tunajipanga kwa ajili ya Simba”-Ettiene

4021
0
SHARE

Na Thomas Ng’itu, Manungu

Kocha w Mbao Etienne Ndyaragije amefunguka kuwa kikosi chake kilikuwa hafifu dhidi ya Mtibwa, baada ya kupoteza kwa mabao mawili kwa moja mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Manungu.

“Tulicheza mpira lakini wenzetu walikuwa bora zaidi yetu,vijana walijitahidi ila Mtibwa walikuwa wametuzidi katika kipindi cha kwanza, lakini nawapongeza vijana kwa kupambana,”Etienne.

Akizungumzia mchezo wao ujao dhidi ya Simba,alisema wanajipanga mapema dhidi ya mchezo huo ili kuweza kupata matokeo wakiwa nyumbani.

“Tumecheza mechi tatu ugenini tumepata pointi tatu,hivi sasa tunachofanya ni kuangalia mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Simba ili tuwe katika nafasi nzuri zaidi,”.

Mbao watacheza na Simba Septemba 21 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here