Home Kitaifa Ngoma kaokoa Jahazi Songea

Ngoma kaokoa Jahazi Songea

5760
0
SHARE

Kwa mara nyingine tena Yanga imeshindwa kupata ushindi kwenye uwanja wa Majimaji wakati ikipambana na Majimaji FC ya Songea na kujikuta ikiambulia sare ya kufungana bao 1-1.

Yanga bado haijapata dawa ya Majimaji

Uwanja wa Majimaji bado umeendelea kuwa mgumu kwa Yanga, katika mechi nne za hivi karibuni za ligi kuu, mabingwa watetezi wamekuwa katika wakati mgumu kwenye uwanja huo

Unaweza ukasema Yanga wanateseka katika dimba la majimaji kwa sababu katika mechi nne walizocheza hivi karibuni, wamefanikiwa kushinda mechi moja huku nyinginetatu zikiwa ni sare.

16/06/2017 Majimamaji 1-1 Yanga

17/01/2017 Majimaji 0-1 Yanga

21/05/2016 Majimaji 2-2 Yanga

05/02/2011 Majimaji 0-0 Yanga

Yanga, Majimaji, sare mbili

Ni sare ya pili kwa Yanga katika mechi tatu ambazo wamecheza hadi sasa, sare zote ni za kufungana 1-1. Walitoka 1-1 na Lipuli kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi kabla ya leo sare ya 1-1 leo dhidi ya Majimaji FC.

Majimaji nao wameoata sare ya pili mfululizo, walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Tanzania Prisons lakini leo wamelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Yanga. Majimaji pia ni miongoni mwa timu ambazo hazijashangilia ushindi katika mechi tatu walizocheza, walifungwa 1-0 na Mbeya City kwenye mechi yao ya kwanza.

Ngoma mzee wa kusawazisha

Katika mechi mbili ambazo Yanga wametoka sare kwa kufunga 1-1, Yanga wamekuwa wakitangulia kufungwa halafu baadae mshambuliaji wao Donald Ngoma anaokoa Jahazi.

Mechi dhidi ya Lipuli walitangulia kufungwa lakini wakasawazisha kupitia kwa Donald Ngoma. Majimaji pia wametangulia kupata lililofungwa na Peter Mapunda lakini baadae Ngoma akaisawazishia Yanga.

Yanga imefikisha poini tano baafa ya kucheza mechi tatu, inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi za Jumamosi September 16, 2017 wakati Majimaji wao wapo nafasi ya 12 wakiwa na pointi mbili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here