Home Kitaifa Safari ya Nduda bado danadana

Safari ya Nduda bado danadana

5058
0
SHARE

Na Thomas Ng’itu

Safari ya kipa wa simba Said Mohammed ‘Nduda’ bado imekuwa kizungumkuti baada ya kutokujulikana siku maalum ya kuondoka kwake kwenda India kutibiwa kama ilivyoripotiwa awali.

Daktari wa timu Yassin Gembe amesema mchezaji huyu bado haijafahamika ataondoka lini kwenda kutibiwa licha ya kuwa taratibu za awali zimeshafanyika.

“Alitakiwa kuondoka muda lakini kuna vitu baadhi nadhani havijakaa sawa, lakini muda wowote na siku yoyote ataondoka kwenda kutibiwa,” Gembe.

Hata hivyo kipa huyo alitua uwanja wa Uhuru asubuhi ya leo na kufuatilia mazoezi ya wenzake, kisha kuzungumza na kocha na daktari huyo na baadaye kuondoka.

Akizungumzia kutokuwepo kwa wachezaji Haroun Niyonzima na Juma Luizio katika mazoezi hayo, alifunguka kuwa wachezaji hao wanaumwa hivyo amewapa mapumziko.

“Niyonzima anaumwa tumbo kwa hiyo nimempumzisha na Luzio pia anaumwa ila sio kwamba majeruhi, Kapombe yeye anafanya mazoezi ya viungo kabla hajaingia uwanjani ili awe fiti zaidi,”.

Naye kocha msaidizi wa timu hiyo Jackson Mayanja, alitamba kikosi chake kipo katika maandalizi mazuri ya kuchukua pointi tatu dhidi ya Mwadui FC mchezo utakaopigwa Jumapili hii Uwanja wa Uhuru, Dar.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here