Home Kimataifa Liverpool warejea mawindoni Champions League, leo tena moto unawaka CL

Liverpool warejea mawindoni Champions League, leo tena moto unawaka CL

4120
0
SHARE

Hawa ndio vinara wa michuano ya Champions League katika ligi kuu Uingereza, hakuna anayewagusa Liverpool kwa idadi ya makombe ya CL wanayo 5, na leo wanaanza kampeni ya kutafuta kombe la 6 watakapowakaribisha Sevilla katika uwanja wa Anfield.

Sheikh Mansoor msimu huu kati ya ndoto zake msimu huu ni kubeba ndoo ya Champions League na uwekezaji wake Man City unaonekana wazi anataka kombe hili, sasa leo nao wanatupa karata yao ya kwanza wakisafiri hadi Uholanzi kuifuata Feyenoord.

Monaco msimu uliopita walicheza vizuri sna katika Champions League lakini safari hii bila Kylian Mbappe, bila Bernardo Silva, bila Tiomue Bakayoko wanawafuata Rb Leizpg nchini Ujerumani kwa mchezo wao wa kwanza.

Tottenham ambao hawana rekodu nzuri katika uwanja wa Wembley lazima watahitaji ushindi ili kuanza kujiweka vizuri katika uwanja huo ambapo hii leo watawakaribisha wababe wa Ujerumani klabu ya Borussia Dortmund.

Mchezo mwingine katika kundi H ambalo linaonekana kuwa moja ya kundi gumu itakuwa kati ya mabingwa watetezi Real Madrid ambao wataikaribisha APOEL Nicosia katika dimba la nyumbani la Santiago Bernabeu.

Fc Porto watakuwa nyumbanu kuwakaribisha Bestikas, Napoli watawafuata Shaktar Donetsk huku Maribor nao watakuwa Ljudski Vrt Stadium kuwakaribisha Spartak Moscow.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here