Home Kimataifa Wangebaki Arsenal hadi leo, basi Champions League wangeiona kwenye video

Wangebaki Arsenal hadi leo, basi Champions League wangeiona kwenye video

3610
0
SHARE

Maisha yanakwenda kasi sana, huwezi kuamini kwamba Alexandre Lacazette, Mesut Ozil na Alexis Sanchez hawashiriki michuano ya Champions League, wachezaji hawa wafuatao kama wangebaki Arsenal hadi sasa baasi nao wasingeshiriki Champions League msimu huu.

Thomas Varmaelen. Kwa sasa anakipiga Barcelona, wakati alipokuwa Arsenal hakuwa na wakati mzuri sana kwani majeruhi yalikuwa yakimuandama lakini baadae akauzwa Barca akaenda Roma kwa mkopo na sasa jina lake lipo katika orodha ya wachezaji watakaoitumikia Barca katika champions league.

Cesc Fabregas. Kati ya usajili unaowauma sana mashabiki wa Arsenal, wakati akiwa Barcelona hawakuwa wanaumia sana kama sasa wanavyomuona kiungo huyu akiwa na jezi ya Chelsea katika michuano ya Champions League huku wao hawapo.

Oxlade Chamberlain. Hana muda mrefu tangia aondoke Arsenal na kujiunga na majogoo wa Liverpool, kama Oxlade asingeenda Liverpool baasi ni wazi msimu huu naye angeiona michuano hiyo katika video tu kama mashabiki wengine.

Wojciech Szczesny. Mlinda lango wa zamani wa Arsenal, hakuea na wakati mzuri sana ndani ya kikosi cha Gunners, msimu huu amejiunga na Juventus japo ni ngumu kupata namba mbele ya Buffon lakini jina la Szczesny lipo katika orodha ya wanaoshiriki Champions League.

Ovie Ejaria. Ana miaka 19 tu kwa sasa, kupata namba katika kikosi cha Liverpool imekuwa ngumu kwake lakini tangu atue kutoka Arsenal kocha Jurgen Klopp amekuwa akimuamini na kumpa nafasi. Jina lake lipo kwenye orodha ya watakaoitumikia Liva katika Champions League msimu huu.

Oguzhan Ozyakup. Alikuwepo benchi wakati Arsenal wanakufa bao 8 kwa 2 kutoka kwa United, baadae aliuzwa akaenda Bestikas ambako maisha yake kisoka yamemnyookea ameshinda makombe ya Uturuki mara 2 na safari hii yupo Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here