Home Kimataifa Mourinho, Shaffih Dauda, wapishana utabiri UEFA Champions League

Mourinho, Shaffih Dauda, wapishana utabiri UEFA Champions League

12841
0
SHARE

Wakati kocha wa Manchester United Jose Mourinho akizipa nafasi Barcelona, Real Madrid, FC Bayern Munich na PSG kufanya vizuri kwenye michuano ya UEFA Champions League huku kukiwa hakuna timu hata moja ya England kwenye orodha yake, Shaffih Dauda amekweda tofauti na kocha huyo.

Dauda anaamini Liverpool ni timu itakayofanya vyema UEFA kati ya timu tano zitakazoiwakilisha England.

England wanaingiza timu tano kwenye ligi ya mabingwa Ulaya Liverpool, Manchester United, Chelsea, Tottenham na Manchester City.

“Katika timu tano za England, mimi naaamini Liverpool watasumbua. Manchester City na Chelsea wanavikosi vizuri lakini Liverpool naona ndio timu ambayo itakuja kuwa-surprise watu wengi,”-Shaffih Dauda.

“Tottenham wapo kwenye kundi gumu lakini nawaona watakuwa na msimu mzuri kutokana na wachezaji wao kama Kane, Dele Ali, kudumu kwa muda kwenye timu yao.”

Real Madrid watachukua Champions League kwa mara ya tatu mfululizo? Barcelona wanakuja kuwajibu Madrid au watakubali wachukue taji la nne katika misimu mitano?

Itakuwa ni zamu ya England kuchomoza tena kufuatia kuwa na uwakilishi wa timu tano au timu kutoka Hispania zitaendelea kunyanyasa? Je ni wakati wa PSG kutimiza kile ambacho matajiri wa timu hiyo wanakitaka?

Maswali yote hayo yatajibiwa kadiri siku zinavyokwenda na timu kuendelea kupungua katika kila hatua ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya kwa ngazi za vilabu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here