Home Kimataifa Messi na Cavanni wavunja rekodi usiku wa Champions league, matokeo yote haya...

Messi na Cavanni wavunja rekodi usiku wa Champions league, matokeo yote haya hapa

15325
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza Lioneil Messi anamtungua Buffon, Barcelona wanaaifunga Juventus bao 3 kwa sifuri huku mabao 2 ya Lioneil Messi yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 59 katika hatua ya makundi tu ya michuano ya Champions League, Ivan Rakitic alifunga bao lingine la Barcelona.

Edson Cavanni naye ameuchukua ufalme wa Zlatan Ibrahimovich ambaye alikuwa na rekodi ya kufunga mabao 20 katika Champions League lakini sasa Cavanni anakuwa na mabao 22 baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Celtic na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa PSG katika michuano ya Ulaya.

Lakini pia Kylian Mbappe ambaye alifunga bao la pili naye sasa anakuwa na mabao 7 katika Champions League mwaka huu na ni Cristiano Ronaldo pekee mwenye magoli mengi kuliko yeye kwani amefunga mabao 10, huku goli la Neymar likimfanta kuhusika katika magoli 11 dhidi ya Celtic.

Mabao hayo na lile la kujifunga la Mikael Lustig liliwafanga PSG kuibuka kidedea na ushindi wa bao 5 kwa bila ugenini dhidi ya Celtic. As Roma wakiwa nyumbani walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Athletico Madrid.

Lukaku alifunga bao lake la 10 katika michuano ya CL hatua ya makundi huku Fellaini akifunga bao lake la 50 tangu aanze kuchezea ligi kuu ya Uingereza, bao la tatu la Manchester United liliwekwa kimiani na Marcus Rashford na mchezo kuisha kwa United kuibuka na ushindi wa bao 3 kwa nunge dhidi ya Fc Basel.

Chelsea waliwapiga vibonde Quarabag Fc bao 6 kwa nunge, bao la Cesar Azipuculeta lilikuwa bao lake la kwanza katika michezo 46 iliyopita aliyoitumikia Chelsea, mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Bakayoko, Batshuayi(2), Zapacosta, na Pedro Rodriguez.

Bayern Munich waliipiga Anderchelt waliocheza pungufu kwa dakika 80 baada ya Sven Kums kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 11 bao 3 kwa 0 huku Robert Lewandoski akifunga bao lake la 50 katika michezo 53 aliyoichezea Bayern tangu msimu uliopita, mabao mengine yalifungwa na Thiago Alcantara huku Joshua Kimmich akifunga la 3.

Benfika wakiwa nyumbani walichezea kipigo cha bao 2 kwa 1 toka CSKA Moscow huku mabao ya  Moscow yakifungwa na Timur na Vitinho, Benfika likifungwa na Saferovic, Olympiacos nao wakiwa nyumbani wakafungamwa 3 kwa 2 na Sporting CP.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here