Home Kimataifa Ukweli kuhusu Alvaro Morata na nyimbo za kumkashifu huu hapa

Ukweli kuhusu Alvaro Morata na nyimbo za kumkashifu huu hapa

13105
0
SHARE

“Tangu nimefika hapa mumekuwa munaniunga mkono kila siku, ninyi ni watu wazuri lakini ningependa kuomba heshima itawale” hiyo ni tweet ya mshambuliaji mpya wa Chelsea kuhusu nyimbo za mashabiki wa klabu hiyo.

Wakati Morata akisema hayo klabu ya Chelsea imetoa onyo kali kwa mashabiki ambao wanaendelea kuimba nyimbo zenye lugha chafu huku kwenye nyimbo hizo jina la Alvaro Morata likihusihwa.

Alvaro Morata na Chelsea wanaonekana kukerwa na nyimbo za mashabiki wa Chelsea lakini ukweli ni kwamba mashabiki hao waliwalenga Tottenham lakini uwepo wa jina lake katika nyimbo hizo ndio jambo ambalo hajalifurahia.

Tayari Chelsea wameawaonya mashabiki zao kuhusiana na nyimbo hizo huku onyo kali likitolewa kwa yeyote atakayekamatwa akiimba nyimbo zisizo na lugha nzuri kuelekea timu nyingine.

Morata ameanza kuwa na maisha mazuri ndani ya Chelsea huku katika mchezo wa juzi dhidi ya Leicester akifunga moja ya bao katika ushindi wa mabao 2 kwa 1 na huku hilo likiwa bao lake la 3 katika Epl tangu atue darajani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here