Home Kimataifa Sekunde 600 zamtosha Ciro Immobile kuteketeza £200m za Ac Millan, avunja rekodi...

Sekunde 600 zamtosha Ciro Immobile kuteketeza £200m za Ac Millan, avunja rekodi ya Shevchenko

8034
0
SHARE

Wakati kampuni la Wachina likiichukua klabu ya Ac Millan na kuwekeza kiasi cha €740m mapema mwaka huu kila mtu aliamini kwamba Ac Millan ya zamani imerudi na kila mtu akaamini utawala mpya wa Millan unakuja.

Usajili wao ulithibitisha ni nini wanataka,ilikuwa wazi wanataka heshima kwani usajili wa €200m huku majina makubwa kama Bonucci, Andre Silva, Ricardo Rodriguez,Andrea Conti,Mateo Muscchio ilionesha wazi Ac Millan wamepania.

Maisha yamekwenda lakini kijana mzaliwa wa jiji la Tore Annazuita miaka 27 iliyopita Ciro Immobile aliwaonesha Ac Millan kwamba pesa zao si lolote na hata hakutumia mda mrefu bali sekunde 600 tu zilimtosha.

Baada ya kushinda michezo miwili ya mwanzo Ac Millan walijikuta hoi katika dimba la Stadio Olimpico huku wakiokota mipira katika nyavu zao mara 3 ndani ya dakika 10 ambazo ni sawa na sekunde 600.

Hii ni mara ya kwanza kuona hattrick katika mchezo kati ya Ac Millan na Lazio tangu Andriy Shevchenko kufanya hivyo mwaka 1999 katika dimba la Stadio Olimpique wakati akiifungia Ac Millan bao kama hizo.

Immobile sio tu kufunga bao hizo 3 kati ya 4 lakini hata bao la 4 la Lazio ni yeye aliyeassist na kuuacha ukuta wa Ac Millan unaoongozwa na beki kisiki Bonucci kutoamini ni nini kinachowatokea.

Immobile ameshawahi kuzichezea Juventus akishindwa kufunga bao hata moja, baadae akaifungia Dortmund bao 3 msimu mzima, wakamuuza Sevilla,akapelekwa Torino alikofunga bao 5 na sasa amerudi Lazio.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here