Home Kimataifa Rafael Nadal ashinda Us Open kwa mara ya tatu

Rafael Nadal ashinda Us Open kwa mara ya tatu

1301
0
SHARE

Hakuna Novack Djokovick, Andr Murray wala Rodger Federer unataraji Rafael Nadal angefanya nini katika mashindano ya US Open kama sio kubeba ubingwa huo kwa mara yake ya tatu.

Ndicho alichofanya Mhispania huyo usiku wa leo katika dimba la Arthur Ashe Stadium akimfunga  Msouth Africa Kelvin Anderson kwa seti 6-3,6-3 na 6-4 katika mchezo uliokuwa wazi kwa Nadal.

Rafael Nadal ilikuwa wazi asingepata upinzani mkubwa kwani wachezaji wote walioko katika 20 bora ya viwango vya tennis walikuwa wameshatoka na sasa ilikuwa yeye na mchezaji namba 28.

Baada ya kushinda Grand Slam mwaka 2013 hii ni Grand Slam nyingine kwa Nadal na inatimiza idadi ya Grand Slam 16 kwa Nadal huku akishinda mbele ya mashabiki wanaompenda kama mwenyeji wa hapo mjini NewYork.

Nadal sasa anakuwa na US Open 3 na kuwa na Grand Slam 16 akimkaribia kinara wa Grand Slam Rodger Federer ambaye hadi sasa ameweka kabatini jumla ya Grand Slam 19.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here