Home Dauda TV Video: Mipango ya FC Barcelona kuhusu dogo wa Tanzania

Video: Mipango ya FC Barcelona kuhusu dogo wa Tanzania

23692
0
SHARE

Na Thomas Ng’itu

Chipukizi Nasry Aziz, anayekipiga katika akademi ya Aspire iliyopo nchini Senegal, amesimulia jinsi ambavyo aliweza kupata nafasi ya kucheza mechi na timu ya Barcelona.

Aziz amesema kutokana na utaratibu wa akademi yao kucheza mechi za kirafiki sehemu mbalimbali, ilikuwa rahisi kwao kucheza na timu hiyo.

“Akademi ile makao makuu yapo Qatar, kwahiyo huwa tunasafiri sana kwenda nchi mbalimbali, Barcelona tulicheza na vijana wao, wana timu A mpaka C kwahiyo tulicheza na vijana wenzetu,” Aziz.

Aziz aliongeza kuwa baada ya kucheza mechi za kirafiki, akademi yao ilipokea taarifa ya vijana watano wanaofatiliwa, yeye pia akiwa miongoni mwa wachezaji hao kitu ambacho anamshukuru Mungu.

Pia anavutiwa na mchezaji Said Ndemla kiungo wa Simba kutokana na aina yake ya uchezaji pindi anapokuwa uwanjani.

“Wapo wachezaji wengi kaka zangu kama Samatta na wengine, lakini Ndemla ni mchezaji anayebadilisha matokeo muda wowote lakini pia anajua kuuchezea mpira”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here