Home Kitaifa Kinachokwamisha Ndemla kwenda kucheza Sweden

Kinachokwamisha Ndemla kwenda kucheza Sweden

8160
0
SHARE

Kiungo mshambuliaji wa Simba Said Hamis Ndemla amepata nafasi ya kwenda kucheza kwenye klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu ya Sweden lakini kuchelewa kwa VISA ndio kunachelewesha safari yake.

Meneja wa mchezaji huyo Almasi Kisongo amesema VISA ndio kitu pekee kinachochelewesha safari ya Ndemla kwenda Sweden kukamilisha taratibu za kujiunga na AFC Eskilstuna .

“Shida kubwa imekuwa ni VISA, mara ya kwanza ubalozi walikataa kwa sababu kulikuwa na matatizo kidogo kwenye ujazaji lakini sasa hivi imepelekwa tena na mtu anaelisimamia hili zoezi ni Said Tuli kwa hiyo sasa hivi tunasubiri”, Almasi Kisongo.

“Nachotaka kufanya sasa hivi ni kumwambia Katibu wa TFF aliingilie kati kwa sababu ni taratibu ambazo huwa anazifanya kwa wachezaji ambao kama kuna tatizo la VISA, watupe barua twende Wizara yenye dhamana ya michezo watupe barua tupeleke ubalozi wa Sweden.”

Klabu anayotarajia kwenda Ndemla ndio klabu anayocheza mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambaye kwa sasa anauguza jeraha la goti baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni huko Afrika Kusini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here