Home Kitaifa “Tumecheza vizuri kuliko Yanga”-Kocha Njombe Mji

“Tumecheza vizuri kuliko Yanga”-Kocha Njombe Mji

4735
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Njombe Mji Mrage Kabange amesema kiufundi timu yao ilicheza vizuri imecheza vizuri zaidi ya Yanga ingawa wamepoteza mechi kwa goli 1-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani

“Licha ya kufungwa bado vijana wetu wamecheza vizuri kuliko Yanga hususan kipindi cha pili na kiufundi tumeridhishwa na kiwango chao, walikuwa wanakosa uzoefu ukilinganisha na wenzetu ambao wana wachezaji wengi wazoefu na wakimataifa,” Kabange.

“Tulipokwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo tuliwaeleza vijana wetu kuwa wacheze mpira bila kujali ukubwa wa Yanga wala majina ya wachezaji wanaocheza dhidi yao ndio maana utaona walicheza vizuri zaidi kipindi cha pili.”

“Goli haliwezi kufungwa bila makosa kufanyika, tulifungwa goli lililotokana na makosa ya golikipa kupanga ukuta wake kabla ya mpira haujapigwa lakini hiyo yote pia inatokana na kukosa uzoefu.”

“Kuna mchezaji wetu aliumia (beki wa kati) akashindwa kuendelea na mchezo, kutokuwepo kwake kulituathiri kwa kiasi kikubwa kiufundi kwa sababu ni mchezaji wetu mwenye kipaji na mwenye nidhamu akiwa kwenye eneo lake.”

Kabange amesema wanaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo kuhakikisha wanafanya vizuri licha ya kupoteza mechi zao mbili za kwanza zote kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here