Home Kimataifa Sababu ya Mourinho kutompa mkono Mark Hughes yafahamika

Sababu ya Mourinho kutompa mkono Mark Hughes yafahamika

13238
0
SHARE

Jana Manchester United walibanwa mbavu, baada ya tambo nyingi na kujitamba kuhusu vipigo lakini jana walikwama na wakawa wapole baada ya kulazimishwa suluhu ya bao mbili kwa mbili na Stoke City.

Mcameroon Choupo Mouting ndio aliwanyamazisha mashabiki wa Manchester United baada ya kufunga mara mbili na kuwafanya United kwa mara ya kwanza msimu huu kumaliza mchezo bila alama 3.

Suluhu ya Manchester United ilikuwa habari lakini habari kubwa nyingine ilikuwa ni tukuo lililotokea baada ya mchezo huo pale Jose Mourinho alipokataa kumpa mkono kocha wa Stoke City Mark Hughes.

Mengi yamekuwa yakizungumzwa, kila mtu akisema hili na yule akisema lile, wengine wanadai suluhu ilimfanya Jose akasirike na kuacha kupeana mkono na Hughea huku wengine wakisema alijisahau.

Lakini habari za uhakika kutoka Uingereza zinasema Mourinho alikasirishwa sana na tukio la Hughes kutaka Mou aadhibiwe kipindi cha pili na ndio maana Mourinho alijihisi kudharauliwa na kuamua kumpotezea.

Kipindi cha pili cha mchezo wa jana kulionekana kuna hali ya mvutano kati ya makocha ambapo inadaiwa Hughes alitaka Mou aadhibiwe,baada ya mchezo huo Mourinho aligoma kabisa kuzungumzia tukuo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here