Home Kitaifa Katwila: Pointi tatu mfululizo zitatuweka kileleni

Katwila: Pointi tatu mfululizo zitatuweka kileleni

2195
0
SHARE
Zubery Katwila (kushoto) kocha mkuu wa Mtibwa Sugar
Na Thomas Ng’itu

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila amesema licha ya kuongoza ligi hivi sasa, bado wanahitaji pointi tatu kila mechi ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye ligi kuu msimu huu.

“Siwezi kusema kuwa nitakuwa bingwa katika ligi kisa naongoza, kikubwa naomba tuwe tunapata pointi tatu kila mechi ili tuwe katika nafasi nzuri ya ligi,” Katwila.

Akizungumzia mchezo huo, amewapongeza Mwadui kwa kucheza vizuri lakini bahati haikuwa upande wao ndio maaana wamepoteza mchezo huo.

“Mwadui walitengeneza nafasi zaidi ya tatu, lakini walishindwa kuzitumia vizuri na sisi tukapata nafasi moja na tukaitumia tukapata bao la mapema na ndio likatupa ushindi.”

Mtibwa imeifunga Mwadui 1-0 na imekuwa ni timu pekee inayoongoza ligi huku ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili mfulilizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here