Home Kimataifa Barcelona yamuingiza matatani Ivan Rakitic

Barcelona yamuingiza matatani Ivan Rakitic

9790
0
SHARE

Croatia wiki iliyopita walikuwa uwanjani kusaka tiketi kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi, walishinda 1 kwa 0 dhidi ya Kossovo lakini baadaye wakapigwa 1 kwa 0 na Uturuki.

Ivan Rakitic alikuwepo katika kikosi cha Crotia kilichofungwa bao 1 kwa 0 na Uturuki lakini hakufanikiwa kumaliza mchezo huo kwani baada ya dakika 50 tu za mwanzo kiungo huyo alitolewa kwa kile kilichodaiwa ni majeruhi.

Lakini hapo jana wakati Barcelona ikiibwagiza Espanyol bao 5 kwa nunge kiungo huyo alikuwepo uwanjani na alionekana fiti 100% huku akifanikiwa kumaliza dakika 90 zote za mchezo huo. 

Jambo hilo limeibua hasira na jazba kwa wananchi wa Crotia wengi wakimshambulia kiungo huyo kupitia mtandao kwamba ni muongo na msaliti asiyelipenda taifa lake ndio maana alidanganya anaumwa.

Gazeti moja la nchini Crotia limetoka na habari ambayo inaongelea Muujiza Wa Rakitic ambapo ndani ya habari hiyo ilikuwa kama kumdhihaki Ractic kwa kuhoji maumivu yake katika timu ya taifa huku akiwa fiti na Barca.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here