Home Kitaifa Rasmi: Imetajwa tarehe ya kuanza Ndondo Cup Mwanza

Rasmi: Imetajwa tarehe ya kuanza Ndondo Cup Mwanza

2189
0
SHARE

Ndondo rasmi jijini Mwanza. Baada ya mashindano ya Ndondo Cup 2017 kumalizika jijini Dar es Salaam sasa ni zamu ya mkoa wa Mwanza  ambapo September 3, 2017 taarifa ilitolewa na Katibu wa chama cha soka mkoa wa huo MZFA Leonard Malongo.

Mlongo ameelezea taratibu za ushiriki Ndondo Cup kwa timu za Mwanza, Ndondo Cup 2018 mkoani Mwanza itazinduliwa rasmi September 20, 2017.

“Ndondo Cup mkoani Mwanza itaanza September 20, 2017 ikianza na wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana, hivyo basi timu shiriki zilizojiandaa zitaanza kuandishwa Jumatatu  September 4, 2017 saa 10:00. Wafike kwenye ofisi za MZFA ili waweze kujiandikisha na kwenda kulipia benki, ada ya ushiriki ni shilingi 300,000.”

“Tutaanza na timu 16 kwa hiyo wajitahidi kuwahi, timu zitakapotia dirisha litafungwa na hakutakuwa na namna nyingine ya kuingiza timu kushiriki michuano ya Ndondo mkoani Mwanza.”

Bingwa wa Ndondo Cup 2017 Mwanza atapata shilingi 3,000,000, mshindi wa pili 2,000,000, mshindi wa tatu 1,000,000, mshindi wa nne 500,000. Mchezaji bora atajipatia shilingi 500,000, golikipa bora 500,000 mwamuzi bora 500,000 na kikundi bora cha ushangiliaji kitapata shilingi 1,000,000.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here