Home Kitaifa Karibu kwangu Ndemla

Karibu kwangu Ndemla

7864
0
SHARE
Said Ndemla (kulia) akishangilia goli lake na Haji Ugando (kushoto) wakati wa mechi dhidi ya Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Kila mtu anamsifia Ndemla, kila mmoja anamwita mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na kila mmoja anamwita kiungo wa kariba ya peke yake Tanzania. Too bad hakuna anayemwona kuwa anadumaa. Alitakiwa kuwa mbali sana mpaka sasa. Ukuaji wake umekuwa hauridhishi na amekosa ukomavu kama mchezaji. Bahati mbaya tunam-treat kama vile bado ni kinda.

 Kipaji anacho lakini hana ukomavu na hili limetokana na kuzoeshwa sifa na washabiki na kukosa watu sahihi (makocha) wa kumsaidia kwenye career development. Watu wanapenda UMACHACHARI wake. Sitoshangaa akianza kupotea kwa sababu kila usajili wa Simba unamuumiza yeye na sisi hatumsihi ajitume zaidi. Inawezekana ana kipaji kuliko Mzamiru, Mo Ibrahim, Kichuya, lakini hawa wamekomaa na wanacheza kwa majukumu kuliko yeye.
 
Na ndicho ambacho hana. Bahati mbaya wanaendelea kusajiliwa akina Okwi, Gyan na Niyonzima na anayeendelea kusogea kutoka hata benchi ni yeye. Nimekumbuka zile zama anahusishwa na Madrid na Sunderland pamoja na Singano. Mwenzie aliwahi kukomaa ila akajisahau, huyu Ndemla hakuwahi kukomaa, amejisahau na hana wa kumfinya sikio.
 
Asante kwa bao zuri la Jumapili. Mimi naitwa Nicasius Kotinyo, na wengi hunambia tunafanana kwa mbali na bahati mbaya sipo karibu na wewe lakini ukikaribia hapa ukasoma utajua ni mimi peke yangu ninayekutizama tofauti na wengi wanaokusifia. Tabu kwelikweli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here