Home Kitaifa Rais wa TFF ametema cheche kwa waamuzi watakaovurunda Simba vs Yanga

Rais wa TFF ametema cheche kwa waamuzi watakaovurunda Simba vs Yanga

2927
0
SHARE

Rais mpya wa TFF Wallace Karia amechimba mkwara kwa waamuzi pamoja na viongozi wa vilabu ambao endapo watapindisha mambo ili kuuharibu mchezo wa Simba na Yanga wa August 23, 2017.

“Tutakuwa wakali mno kwa wasimamizi wa mchezo huo pamoja na viongozi wa vilabu ambao watajaribu kufanya njia zozote za hila ili kupata ushindi nje ya taratibu halali. Hatutasita kumpoteza mwamuzi kwenye masuala ya michezo kama ataleta mchezo na mchezo wa kesho,” Wallace Karia-Rais wa TFF.

“Waamuzi tuliowachagua wako makini na wanauwezo, watakapofanya makusudi yoyote na sisi, wataona makusudi yetu.”

Mechi za hivi karibuni za Simba dhidi ya Yanga zimekuwa zikimalizika huku waamuzi wakiishia kubebeshwa mizigo ya lawama kwa kushindwa kumudu mechi husika huku baadhi ya waamuzi wakiishia kufungiwa au kusimamishwa.

Karia ameingia madarakani August 12, 2017 baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa TFF uliofanyia mkoani Dodoma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here