Home Kimataifa Wiki ya pili tu, Mourinho aonesha dalili ya ubingwa Epl

Wiki ya pili tu, Mourinho aonesha dalili ya ubingwa Epl

7540
0
SHARE

Frank Lampard alipostaafu soka na kuanza kuwa mchambuzi alikiri ya kwamba Jose Mourinho ni kocha ambaye anawafanya wachezaji wajihisi kama washindi, ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo anawafanya wajione tayari wameshinda.

Jose Mourinho amebeba makombe mengi ya Epl ambayo wiki tatu za mwanzo aliongoza ligi na hiyo imekuwa kawaida kwake toka akiwa Chelsea, kama unakumbuka wakati anarejea Chelsea alikaa kileleni Jumatatu ambayo waliifunga Burnley 3-1 na kuanzia hapo hakushuka hadi wanabeba kombe.

Katika makombe matatu ambayo Mourinho aliwapa Chelsea, yote kuna kipindi ndanj ya miezi mitatu ya mwanzo alikaa kileleni na hata kama alishuka baasi alirudi tena na kukaa kileleni hadi ligi imemalizika na hivi leo tunavyoongea yupo kileleni.

Hajawahi Mourinho kuongoza ligi mwanzo mpaka inaisha lakini mara nyingi amekuwa akiongoza na kushuka lakini akirudi kileleni tena amekuwa akikaa kwa muda mrefu hadi ubingwa unapopatikana.

Kama haujui tu mara ya mwisho Manchester United kuanza msimu kwa moto kama huu ilikuwa msimu wa mwaka 1907/1908 baada ya kuifunga Aston Villa 4-1 na mechi iliyofuata wakaipiga Liverpool 4-0 lakini safari hii wamepiga 4-0, 4-0.

Maeneo mengi yaliyokuwa na matatizo msimu uliopita yanaonekana kuzibwa, uwepo wa Mkhitaryan aliyetoa assist 4,eneo la ulinzi lisiloruhusu bao na kuwa na mabao 8 ya kufunga inaweza kukupa picha jinsi Manchester United walivyo sawa msimu huu.

Kama unakumbuka msimu uliopita kulikuwa na maswali mengi, Pogba anastahili kununuliwa kwa bei aliyonunuliwa? Wayne Rooney anasatahili kubaki United? Eneo la ulinzi liko sawa? Je Zlatan anafunga kutokana na nafasi? Maswali ambayo msimu huu kuna kila dalili yasisikike.

Tayari kuna tetesi kwamba Zlatan Ibrahimovich anarejea Manchestet United, hii inaweza kukupa taswira mpya ya kutisha sana kuhusu eneo la ushambuliaji la Manchester United msimu huu endapo Kadabra atarudi.

Zlatan kucheza na Romelu Lukaku mbele ni jambo ambalo hakuna beki wa timu pinzani angependa kulisikia, ni kama ndoto ya kutisha sana. Kama unakumbuka Kadabra alikiri PSG alikuwa na msimu mzuri zaidi, lakini unajua sababu? Sababu ni uwepo wa Edson Cavanni kule PSG.

Kadabra anahitaji mtu mwingine shupavu kama yeye kucheza nae eneo la ushambuliaji, Lukaku ni mti sahihi kwake, kama Unite hawatakuwa na majeraha mengi kama msimu uliopita kuna kila dalili msimu huu Old Traford pakawa machinjio ya wapinzani na kutokana na jinsi Mou alivyotwaa makombe ya Epl yaliyopita anaonekana na mwaka huu yuko njia hiyo hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here