Home Kimataifa La Liga’s Back: Madrid wanaisaka rekodi bora ya ufungaji ya Santos ya...

La Liga’s Back: Madrid wanaisaka rekodi bora ya ufungaji ya Santos ya Pele

6559
0
SHARE

Real Madrid wanaendelea kuwa timu ya aina yake kila siku, wakishinda taji baada ya taji chini ya uongozi wa Zinedine Zidane, na sasa wana changamoto ya kuivunja rekodi nyingine mbele yao: kuvunja rekodi ya kufunga katika mechi 74 mfululizo iliyowekwa na klabu ya Santos ya Brazil.

Klabu hiyo ya Brazil waliiweka hii rekodi mwaka 1960, lakini sasa Los Blancos wanashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee ya ulaya ambayo ina rekodi ya kufunga katika mechi 68 mfululizo.

Vijana wa Zidane wanahitaji katika mechi 6 tu mfululizo zijazo ili kuifikia rekodi ya Santos kuanzia mchezo ujao wa ligi vs Deportivo La Coruna mpaka dhidi ya Real Betis katika uwanja wa Santiago Bernabeu. september 20.

Kabla ya mchezo huu, timu pekee ambayo inaonekana itawapa ugumu ni Valencia – ambao waliwafunga Madrid msimu uliopita katika uwanja wa Mestalla mwezi February.

Kipigo hicho vs Valencia kilikuwa ni kimojawapo kati ya vitano ambavyo Madrid wamefungwa katika mechi 68 za mashindano zilizopita – timu nyingine zilizowafunga Madrid ni Sevilla, Celta Vigo, Barcelona na Atletico Madrid.

Santos wao waliweka rekodi ya kushinda mechi 51 katika mechi 74 walizofunga mfululizo, walitoka sare 14 na kupoteza 9. Madrid katika mechi zao 68 walizofunga mfululizo wameshinda idadi sawa na Santos, mechi 51, sare 12 na wamepoteza 5.

Santos walifunga magoli 245 katika mechi hizo 74 walizofunga mfululizo, Madrid wamefunga magoli 186 katika mechi 68 walizofunga mfululizo – 42 kati ya magoli hayo yalifungwa na Cristiano Ronaldo.

Madrid wanakipiga vs Deportivo La Coruna – Je wataendelea na kuisaka rekodi ya Santos au Deportivo wataikatisha? Majibu yote tutayashuhudia on AZAM TV jumapili ijayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here