Home Dauda TV Hivi ndivyo watu walivyouawa Barcelona na hii ni video Shaffih Dauda alipoenda...

Hivi ndivyo watu walivyouawa Barcelona na hii ni video Shaffih Dauda alipoenda eneo la tukio

10650
0
SHARE

Wingu zito limetanda katika jiji la Barcelona jiji ambalo inatokea klabu ya FC Barcelona baada ya shambulizi la kigaidi kutokea katika eneo la kitalii la Las Ramblas. Shambulizi hilo limeua watu 13 huku wengine 100 wakijeruhiwa.

Magaidi hao walitumia gari la mizigo kutekeleza shambulio hilo ambapo waliendesha gari hilo kwa nguvu kuelekea sehemu ambapo kulikuwa na umati mkubwa wa watu na kuwagonga.

Ripoti toka barani Ulaya zimekitaja kikundi cha Islamic State kuhusiana na tukio hili la kigaidi huku mashuhuda wakisema ilikusudiwa kuua watu wengi sana.

Wakati shambulio hilo linatokea kulikuwa na timu za kikapu za vyuo za Oregon State, Tulane, Arizona na Grand Canyon zilikuwepo karibu na eneo la tukio lakini hakuna alieyeumia.

Kutokana na shambulio hilo la Barcelona polisi walifanya msako kuwatafuta magaidi ambapo walifanikiwa kuua magaidi watano kama ripoti za polisi wa Catalan zinavyosema.

Shaffih Dauda mwaka huu alifanikiwa kufika mji huu wa Barcelona ambapo ndipo shambulizi limefanyika na kuongea na baadhi ya wenyeji wa eneo hili, tujikumbushe safari yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here