Home Dauda TV Video: Katibu Mkuu wa Yanga ametoa ufafanuzi kuhusu jengo lao kupigwa mnada

Video: Katibu Mkuu wa Yanga ametoa ufafanuzi kuhusu jengo lao kupigwa mnada

10258
0
SHARE

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Biniface Mkwasa ametoa ufafanuzi kuhusu madai ya jengo la klab hiyo kupigwa mnada kutokana na deni la zaidi ya shilingi milioni 300 la malimbikizo ya kodi ya ardhi tangu mwaka mwaka 1996 hadi sasa.

“Mkwasa amekiri kwamba Yanga ina deni la kodi ya ardhi kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari Ni kweli tuna tatizo ambalo limejitokeza tangu mwaka 1996/97 kutokana na matatizo yetu na changamoto nyingi ambazo zimeikumba klabu hii, ulipaji wake umekuwa una suasua hadi mwaka huu,” Mkwasa.

“Tumeshaandika barua Wizarani kuomba kibali cha kupunguza au kuondoa intrerest ¬†ili kuweza kulipa lakini mawakala ambao wamepewa jukumu la ¬†kukusanya mapato ya serikali wanadai kwa sababu na wao wana asilimia 10 ya kuksanya.”

Leo Augst 17, 2017 asubuhi, ilisambaa taarifa ya jengo la Yanga kupigwa mnada huku tayari tangazo rasmi likiwa limeshatoka ili jengo hilo liuzwe kufidia kodi ambayo Yanga inadaiwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here