Home Kitaifa Mkomola ameenda Tunisia kukamilisha dili

Mkomola ameenda Tunisia kukamilisha dili

5442
0
SHARE

Mshambuliaji wa Serengeti Boys Yohana Mkomola na wenzake wawili wamesafiri leo August 17, 2017 kwenda nchini Tunisia kwenye klabu ya Etoile du Sahel. Mkomola alishafuzu majaribio ya kujiunga na klabu hiyo lakini wenzake wawili wameitwa kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu.

Kocha wa kituo cha soka cha Cambiaso Sports Center Ngawina Ngawina kpitia Sports Extra ya Clouds FM amethibitisha kuondoka kwa vijana hao kwenda nchini Misri.

“Kweli Mkomola ameondoka leo alfajiri alikuwa na wenzake wawili kwenda Etoile du Sahil. Mkomola tayari alishakwenda awali na akafuzu majaribio lakini wenzake wawili (Henriq Vitalis na Ally Ng’anzi) wanakwenda kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu,” Ngawina Ngawina.

“Mualiko wao ulikuja wakati wanatakiwa kujiunga na timu ya taifa kwa hiyo wakaambiwa wasubiri lakini sasa hivi wameshamaliza majukumu ya Serengeti Boys na wao wanakwenda kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu.”

“Mkomola anakwenda kwa ajili ya mkataba lakini atasubiri kwa muda hadi afikishe miaka 18 ili asaini mkataba lakini kwa sasa atakuwa kwenye academy ya Etoile du Sahil. Hao wengine endapo watafuzu watajinga na academy kabla ya kusaini mikataba hadi watakapotimiza miaka 18.”

Awali taarifa za Mkomola kuelekea Tunisia zilianza kusambaa baada ya yeye mwenyewe ku-post picha akiwa uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here