Home Kimataifa Neymar na PSG waokoa kiwango cha Paul Pogba

Neymar na PSG waokoa kiwango cha Paul Pogba

15296
0
SHARE

Msimu uliopita wa ligi ulikuwa mgumu sana kwa Paul Pogba kutokana na usajili wake Manchester United, kila mtu alikuwa akihoji kuhusu ada ya uhamisho wake na kile anachokifanya uwanjani.

Mashabiki wengi wa soka walumbebesha zigo la lawama Pogba wakidai hastahili kuwa mwanasoka anayeshikilia rekodi ya usajili duniani.

Maisha yameenda lakini zigo alilolibeba Pogba msimu uliopita la rekodi ya usajili sasa limebebwa na Neymar Dos Santos aliyeenda PSG kwa ada ya £196m.

Pogba mwenyewe amekiri kwamba siku hizi baada ya usajili wa Neymar kwenda PSG amekuwa akiulizwa sana kuhusu soka lake na sio pesa ya usajili kama msimu uliopita.

“Msimu uliopita swali la kwanza lilikuwa pesa ya usajili wangu lakini siku hizi kila mtu ananiuliza kuhusu soka hilo ni jambo zuri na inanipa kujiamini zaidi katika msimu huu” alisema Pogba.

“Nilipokuwa hapa mara ya kwanza nilitamani sana kucheza lakini sikuwa timu ya kwanza, nilipokuwa Italia nimekua sana na sasa nimerudi kama mwanaume nina furaha sana” aliongeza Pogba.

Paul Pogba anaonekana ameanza kuwa free zaidi na kuanza kuonekana akicheza vizuri tangu United wamnunue Nemanja Matic huku kiungo huyo akifanikiwa kufunga katika mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya WestHam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here