Home Dauda TV Shaffih Dauda na Ally Mayay baada ya kushindwa uchaguzi

Shaffih Dauda na Ally Mayay baada ya kushindwa uchaguzi

7232
0
SHARE

Baada ya uchaguzi mkuu wa TFF kumalizika na kupata viongozi wapya watakaohudumu kwa miaka minne, wadau wengi wanatamani kusikia chochote kutoka kwa washindi pamoja na wale walioshindwa.

Shaffih Dauda na Ally Mayay ni miongoni mwa wagombea walioshindwa kwenye uchaguzi uliomalizika. Dauda alikuwa anagombea ujumbe wa kamati ya utendaji kupitia Kanda ya Dar es Salaam na Ally Mayay yeye alikuwa anawania urais wa TFF.

“Uchaguzi umemalizika kilichobaki ni sisi kuwaunga mkono waliochaguliwa kwa sababu lengo la wote lilikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya mpira wa Tanzania,” Shaffih Dauda.

“Haiwezekani watu wote tuwe wajumbe wa kamati ya utendaji, kuna nafasi kadhaa zimeandaliwa ┬álakini wote ambao tulikuwa tumejitokeza lengo letu lilikuwa moja. unaweza ukiaona watu wote waliotoa sera kila mtu anazngumzia maendeleo ya soka la vijana, miundo mbinu, tawala bora kwa hiyo wote walikuwa na nia moja na sisi tupo nyuma yao.

“Sisi ndio waasisi wa mpira wa miguu na dhana na ‘fair play’, unafungwa magoli 9-0 na unaondoka na kwenda kumuunga mkono aliyekufunga mnakaa pamoja na kunywa wine,” Ally Mayay.

“Tunashukuru sana wajumbe kwa uchaguzi na tumemaliza vizuri kamati imesimamia uchaguzi ulikuwa huru na haki, mambo yamekwenda vizuri watu wamezungumza content. Uchaguzi ulikuwa fair na tunaunga mkono.”

“Kabla ya uchaguzi tulikuwa tunafanya kazi ya mpira na tutaendelea kufanya kazi ya mpira na viongozi waliochaguliwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here