Home Dauda TV Wambura baada ya kushinda, Ng’hambi baada ya kushindwa uchaguzi wa TFF

Wambura baada ya kushinda, Ng’hambi baada ya kushindwa uchaguzi wa TFF

3635
0
SHARE

Dauda TV imememnasa mshindi wa nafasi ya makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ambaye ameshinda kwa kishindo baada ya kupata kura 85 katika uchaguzi.

Wambura amesema uchaguzi wa mwaka huu ulikwenda vizuri ukilinganisha na chaguzi nyingine ambazo zimepita na kuishia kulalamikiwa na wagombea kutokana na kutokuwepo kwa haki.

“Mchakato umekwenda vizuri, uchaguzi umeandaliwa vizuri taratibu zimefuatwa na process nzima ya Democrasia imechukua nafasi yake lakini miaka ya nyuma kulikuwa na figisu mara huyu kakatwa mara huyu kafanya hivi.”

“Tulichojifunza ni kwamba Democrasia ikisimamiwa vizuri uchaguzi unaweza kwenda bila malalamiko yoyote.”

Kwa upande wa mgombea wa nafasi ya makamu wa Rais ambaye ameshindwa kwenye uchaguzi huo Mulamu Ng’hambi amesema, badoa ni kijana hivyo hakati tamaa licha ya kushindwa.

“Sijawahi kusisima, mimi bado kijana tuendelee kuomba Mungu atupe uhai tutaendelea kusaidia katika mpira hadi hapo tutakapoona tunataka kwenda katika njia gani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here