Home Dauda TV Jambo la kwanza atakaloanzanalo Rais mpya wa TFF Wallace Karia

Jambo la kwanza atakaloanzanalo Rais mpya wa TFF Wallace Karia

4565
0
SHARE

Rais mpya wa TFF Wallace Karia amesema, ataanza kwa kufanya marekebisho ya watendaji wa TFF kuanzia muundo lakini pia ameahidi kurebisha mapungufu ya utendaji yaliyopo kwa kushirikiana na kamati ya utendaji.

“Nitaanza na marekebisho kwenye secretariat kuanzia muundo, lakini kesho tutakutana na kamati ya utendaji tutaanza kuweka vipaumbele kwa pamoja kwa sababu mimi nina mawazo yangu lakini tutashirikiana kuona tuanze na lipi katika utekelezaji.”

“Kuna mapungufu kwenye masuala ya utendaji ambayo lazima tuyarekebishe ili tuweze kupata watu ambao wana sifa na wanao stahili kwenye ofisi yetu ya TFF.”

Alipoulizwa kuhusu kuachia nafasi aliyonayo serikalini Karia amejibu kwamba, nafasi aliyonayo haimzuii kutekeleza majukumu yake kama Rais wa TFF kwa sababu yeye sion mwajiriwa wa shirikisho na badala yake yeye ni msimamizi wa secretariat.

Karia ni mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa mkoa Morogoro anakohudumu hadi sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here