Home Kimataifa Huddersfield town waitoa Arsenal kileleni EPL, mabingwa watetezi wakidhalilika

Huddersfield town waitoa Arsenal kileleni EPL, mabingwa watetezi wakidhalilika

6427
0
SHARE

Michezo 7 mingine ya Epl imepigwa hii leo ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Liverpool dhidi ya Watford ambapo mchezo uliisha kwa sare ya bao 3 kwa 3.

Walianza Watford dakika ya 8 kupitia kwa Okaka Chuka kabla ya Mane kuisawazishia Liverpool,Dakika ya 32 Doucoure aliiandikia Watford bao la pili ambapo Firminho alisawazisha dakika ya 55.

Baadae Mohamed Salah aliifungia Liva bao dakika ya 57 na kuwaoa Liva matumaini ya kubeba alama 3 lakini ilipofika dakika ya 90 matokeo yalibadilika baada ya Miguel Bristos kuisawazishia Watford.

Chelsea wakiwa darajani waliabika baada ya Burnley kuwachapa bao 3 kwa 2 huku mchezo huo Chelsea wakiumaliza pungufu baada ya Garry Cahil na Cesc Fabregas kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Burnley walitangulia kwa mabao 3 kipindi cha kwanza yakifungwa na Sam Vokes aliyefunga mawili na Stephen Ward akifunga moja huku mabao ya Chelsea yakifungwa na Alvaro Morata na David Luiz.

Wayne Rooney ameendelea kufumania nyavu baada ya kuifungia Everton bao pekee katika mchezo dhidi ya Stoke City huku Swansea na Southampton wakitoka suluhu ya bila bila.

Wageni katika ligi Huddersffield Town waliishangaza Crystal Palace iliyokuwa nyumbani baada ya kuwafunga mabao 3 kwa 0 huku bao la Ahmed Hegazy akiifunga West Bromich bao pekee katika ushindi wao dhidi ya Fc Bournamouth.

Manchester City walikuwa wageni wa Brighton Albion na wakashinda 2 kwa 0, mabao ya Kun Aguero na lile la kujifunga la Lewis Dunk huku matokeo ya leo yakiipeleka Huddrsfield Town kileleni mwa ligi kwa tofauti ya mabao.

Hapo kesho kutapigwa mitanange miwili ambapo Tottenham Hotspur watacheza dhidi ya Newcastle United watakaokuwa nyumbani huku Manchester United wakiikaribisha West Ham United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here