Home Kimataifa Ubingwa unakwenda Manchester au London?huu ndio utabiri wangu wa Epl 2017/2018

Ubingwa unakwenda Manchester au London?huu ndio utabiri wangu wa Epl 2017/2018

14285
0
SHARE

Pazia la ligi kuu nchini Uingereza linafunguliwa rasmi hii leo, mashabiki duniani kote wamekuwa wakisubiria msimu huu kwa hamu kubwa sana kwani timu nyingi zinaonesha matumaini ya kufanya vizuri msimu huu.

Mbio za ubingwa zinaweza kuwa ngumu zaidi kuliko msimu uliopita, kwani makocha wawili vigogo Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Gurdiola hawawezi kukubali kutochukua Epl mara ya pili lakini Wenger anataka kurudisha heshima huku Conte akitaka kuendeleza utemi.

Chelsea, kwa upande wangu siamini sana kama Chelsea wanaweza kuchukua tena kombe msimu huu. Hakuna uhakika wa mabao aliyofunga Diego Costa yakapatikana tena msimu huu na hii inanipa uhakika kuamini kasi ya ufungaji ya Chelsea itapungua sana.

Ngolo Kante amechukua Epl mara mbili mfululizo huku mara zote akiwa muhimu na hii inaweza kumfanya awe ametumika sana na kumpelekea kuchoka, msimu huu tunaweza tusimuone Kante wa msimu uliopita, nawapa 50% kuchukua ubingwa.

Arsenal, ni kweli Lacazette atawasaidia Arsenal kufunga na idadi ya mabao itaongezeka, lakini je Arsenal wana tatizo la ufungaji tu? Jibu ni hapana, tangu kuondoka kwa kizazi cha Patrick Viera tatizo la kiungo haswa mkabaji limekuwa kubwa kwao.

Granit Xhaka ni mzuri na ana uwezo mkubwa lakini nidhamu yake ni mbovu na huwezi muamini anaweza kuitumikia Arsenal katika michezo mingi, na Arsenal wamekuwa na tatizo la kukosa wachezaji wakubwa kupambana ila kutokuwepo kwao katika Champions League kunanifanya niwape 45% za kubeba kombe.

Manchester City, bila kupepesa maneno hawa nawapa asilimia nyingi za kuwa mabingwa msimu huu, tayari katika makaratasi tu kikosi chao kinaonesha kinataka nini, ni ubingwa tu na naamini safari hii wapinzani watapata tabu sana kuikabili Man City.

Maingizo ya Kyle Walker, Bernado Silva,Benjamin Mendy,Danilo na golikipa Ederson ni usajili ambao unaweza kufukia makosa ya kiuchezaji ambayo yaliicost sana City msimu uliopita haswa eneo la ulinzi.

Gabriel Jesus tayari aliionesha dunia uwezo wake wa kucheka na nyavu na uwepo wa Kun Aguero unaweza kuifanya City kuzidi kutikisa nyavu za wapinzani wao katika ligi, nawapa 75% kubeba ndoo.

Manchester United, sio rahisi kwa kocha mshindani kama Jose Mourinho kukubali kukosa kombe la Epl ndani ya misimu miwili na msimu huu kombe linakwenda jiji la Manchester wakilikosa City watachukua United.

Sahau kuhusu ujio wa Lukaku ambaye nina uhakika atafunga sana msimu huu lakini ujio wa Matic unaweza kukifanya kiungo cha Manchester United kuwa imara na kucheza vizuri zaidi msimu huu kuliko uliopita, nawapa 68%.

Tottenham Hotspur, wamefanikiwa kubakiza karibia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza kasoro Kyle Walker na kama kuna timu kutoka nje ya Manchester itayoleta changamoto baasi ni Tottenham Hotspur.

Muunganiko wao na discpline waliyonayo kiuchezaji imekuwa ikileta changamoto kubwa sana kwa misimu miwili mfululizo, wataendelea kubaki kuwa washindani lakini ubingwa bado ni mgumu kwao, nawapa 55%.

Liverpool, tetesi za Phellipe Coutinho kuondoka zinazidi kushika kasi, endapo Mbrazil huyo ataondoka litakuwa pigo kubwa sana kwao kwani amekuwa chachu na injini kubwa ya uchezaji wa Liverpool.

Ujio wa Mo Salah na fomu ya kinda Solanke vinaweza kuleta kitu kipya ndani ya Liverpool, aina yao ya uchezaji wa kasi inaweza kuongezeka na wakawa katika fomu kupita msimu uliopita nawapa 57% kuchukua ndoo.

Tishio, kama uliwaona Leicester City walivyochukua kombe hakuna mtu alieyedhania na walileta changamoto kubwa mnoo kwa vigogo wa ligi kuu nchini Uingereza na kubeba ndoo.

Sasa msimu huu watizame West Ham, waangalie na Everton kwa jinsi usajili wa vilabu hivyo viwili ulivyofanyika sitashangaa mmoja kati ya timu vigogo wa Epl akamaliza ligi chini ya Everton au Westham au chini ya wote wawili.

Kwa usajili ulivyo hadi sasa nikiulizwa kuweka orodha ya timu 4 zitakazomaliza juu naamini City watakuwa mabingwa, United namba 2, Liverpool namba 3, na Tottenham watamaliza nafasi ya 4, haya ni maoni yangu mimi kama mwandishi yanayochagizwa na uzoefu wangu katika kuangalia Epl.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here