Home Kimataifa Morata akiri pesa alizonunuliwa nazo zinamtesa

Morata akiri pesa alizonunuliwa nazo zinamtesa

5659
0
SHARE

Mshambuliaji Alvaro Morata alinunuliwa Chelsea huku mashabiki wa klabu hiyo wakiwa na matumaini makubwa sana kutoka kwa Mhispania huyo.

Dau la £70m lilitumika kumchomoa Morata Real Madrid huku Chelsea wakiwa na matumaini kwamba Morata atakuwa mbadala wa Diego Costa aliyeko mbioni kutimka.

Toka ajiunge na klabu ya Chelsea Morata hajafanikiwa kufunga goli na kitendo cha kukosa penati dhidi ya Arsenal kilizidi kuleta minong’ono juu ya mshambuliaji huyo.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amewataka mashabiki wampe muda Morata lakini Morata mwenyewe ameshaanza kuona presha ilivyo kubwa katika klabu ya Chelsea.

“Ni kweli pesa niliyosajiliwa nayo ni kiasi kikubwa cha fedha lakini hiyo ndio inanipa hamasa kupambana na naelewa sana mashabiki wanataka nini kutoka kwangu” alisema Morata.

“Nimecheza michezo miwili tu ya pre season na nikacheza dakika 15 dhidi ya Arsenal lakini nilipokosa penati watu walitaka kuniua na najua ni kwanini”

Lakini Morata amewaahidi mashabiki wa Chelsea kwamba msimu huu ana malengo ya kuhakikisha atafunga mabao zaidi ya 20 na amepania sana kufanya hivyo.

“Ninataka kufunga mabao zaidi ya 20 lakini kubwa ni kuisaidia timu kubeba ubingwa kwani wakati nipo Juve sikufunga mabao zaidi ya 20 ila timu ilibeba kombe la ligi.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza wataanza kampeni yao ya kutetea ubingwa wao hapo kesho wakiwq nyumbani dhidi ya Burnley.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here