Home Kimataifa Arsenal waistaajabisha Leicester City huku Lacazette akiweka rekodi ya kwanza Epl

Arsenal waistaajabisha Leicester City huku Lacazette akiweka rekodi ya kwanza Epl

12889
0
SHARE

Hakika hiki ndicho kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa soka, utamu wa ligi ya Epl na leo umeanza kuonekana kwa mechi kali mno ya ufunguzi.

Dakika ya 2 tu ya mchezo goli la kwanza lilipatikana baada ya Alexandre Lacazette kuiandikia Arsenal bao la kwanza na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao Epl 2017/2018, lakini dakika 3 baadaye Leicester walisawazisha kupitia Shinji Okazaki.

Pande zote mbili ziliendelea kushambuliana na dakika ya 29 Jamie Vardy akaifungia Leicester bao la pili kabla ya Danny Welbeck kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na mchezo kwenda mapumziko kwa sare.

Kipindi cha pili dakika ya 56 Jamie Vardy tena aliitanguliza Leicester City na hadi dakika ya 82 Leicester walikuwa wanaongoza kwa mabao 3 kwa 2 na mashabiki wa Arsenal wakaanza kuchanganyikiwa.

Lakini ilipofika dakika ya 83 zikiwa ni 7 kabla ya mchezo huo kuisha Aron Ramsey aliisawazishia Gunners na watu kuanza kuaminu Arsenal wamebahatika kupata sare, dakika 5 kabla ya mchezo kuisha Olivier Giroud aliwapa Gunners raha alioifungia bao la 4.

Goli la Giroud limemfanya kufikisha idadi ya magoli 50 katika uwanja wa Emirates na sasa ni Robina Van Persie (65) na Theo Walcott (54) wenye mabao mengi kuliko Giroud katika uwanja wa Emirates.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here