Home Kitaifa Ni Shilawadu vs Clouds 360 katika fainali ya Ndondo Cup

Ni Shilawadu vs Clouds 360 katika fainali ya Ndondo Cup

3042
0
SHARE

Ni Misosi vs Goms (Clouds 360 vs Shilawadu) katika fainali ya aina yake ya michuano ya Ndondo Cup 2017.

M-cheza bado wameendelea kuipa nguvu Ndondo Cup kwa kutoa zawadi kwa timu zinazoshinda, zinazofungwa na mchezaji bora wa mechi tangu hatua ya 16 bora hadi mechi ya fainali.

Leo August 10, 2017 uimepigwa nusu fainali ya pili ya Ndondo Cup kati ya Kibada One dhidi ya Goms United mchezo ambao umeshuhudia Goms ikitinga fainali baada ya kupata ushindi wa 2-0 walioupata kwa kuwachapa Kibada One.

Goms watacheza na Misosi katika fainali ya msimu wa nne wa michuano ya Ndondo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza.

Pambano la fainali linavihusisha vilabu vya wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Misosi (Kinondoni) vs Goms (Ilala) wakati huo likiwa ni pambano la vipindi viwili vya Clouds TV (Clouds 360 vs Shilawadu).

Utakumbuka kwamba, kuanzia hatua ya 16 bora vipindi mbalimbali vya Clouds Media Group viliingia kutoa support kwa timu ambazo zilifuzu hatua hiyo. Vipindi vyote vya radio vimepigwa chini na kuviacha vipindi viwili vya TV vikikutana fainali.

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itachezwa na timu zilizofungwa kwenye nusu fainali ambazo ni Keko Furniture vs Kibada One.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here