Home Kitaifa Hadi Mkude, Nduda, walikuwepo Ndondo Cup

Hadi Mkude, Nduda, walikuwepo Ndondo Cup

5454
0
SHARE

Fundi wa golini Said Mohamed ‘Nduda’ na fundi wa dimba la kati Jonas Mkude ambao wote ni wachezaji wa Simba, walikuwepo uwanja wa Kinesi kushuhudia nusu fainali ya Ndondo Cup kati ya Goms United vs Kibada One.

Jonas ni kiungo ambaye anaendelea ktamba na klabu ya Simba na timu ya taifa akiwa anafanya vizuri katika nafasi anayocheza akiwa uwanjani. Wakati Nduda ni mshindi wa tuzo ya golikipa bora wa michuano ya COSAFA 2017 ambae amesajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota hao walionekana kufatilia mechi ya Ndondo kwa umakini mkubwa na huenda walikuwa wakivutiwa na aina ya mechi lakini pia baadhi ya wachezaji wa timu zote mbili zilizokwa uwanjani.

Wapo mastaa kibao wa ligi kuu ambao mara kadhaa wamekuwa wakifatilia mashindano hayo, Amisi Tambwe, Juma Abdul, Shiza Kichuya, Said Ndemla nni baadhi yao huku wengine wakishiriki kabisa kwa kucheza kwenye michuano hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here