Home Kimataifa Borussia Dortmund na Liverpool zaendelea kuiliza Barcelona

Borussia Dortmund na Liverpool zaendelea kuiliza Barcelona

5084
0
SHARE

Baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wao Neymar Dos Santos klabu ya Barca imekuwa ikihangaika sana kwa ajili ya kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Neymar aliyekimbilia PSG.

Kiasi cha £196m walichopokea kutoka kwa matajiri wa PSG kinawafanya wawe katika nafasi nzuri ya kununua mchezaji mpya kutoka popote pale.

Phellipe Coutinho alikuwa mmoja wa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa kuchukua nafasi ya Neymar huku pia akitajwa kama mrithi ajaye wa Iniesta.

Barcelona walituma ofa ya kwanza ya £70m kwa Liverpool ambapo Liva waliikataa, wakatuma tena £80m ikakataliwa na hawakuchoka hii leo Liverpool wameikataa ofa yao ya 3 ya £90m.

Hii leo Coutinho aliwasili Melwood kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza huku kocha wake akisema mchezaji huyo ana furaha kuwa Liverpool.

Jurgen Klopp amesisitiza kwamba klabu yake haina mpango wa kumuuza mchezaji yoyote kwa sasa “hakuna atakayeondoka, tunataka kuwa na wachezaji bora na kuwabakisha tulionao” alisema Klopp.

Wakati Klopp akisema hivyo, Barca wakaona sio kesi ni bora waende Ujerumani na kujaribu kuongea na klabu ya Borrusia Dortmund kuhusu Osmane Dembele.

Dortmund nao wamewatosa Barcelona na kisema Dembele ni muhimu katika klabu yao na kusema kwa sasa mazungumzo kati yao na Barca yamekufa.

Kuhusu taarifa za Dembele kutotokea mazoezini klabu ya Dortmund imeamua kumuadhibu kwa kumfungia mchezaji huyo wiki nzima na pia adhabu hiyo itaambatana na faini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here