Home Dauda TV Video: Penati 19 mechi moja zimeweka rekodi Ndondo Cup 2017

Video: Penati 19 mechi moja zimeweka rekodi Ndondo Cup 2017

3098
0
SHARE

Mechi ya nusu fainali ya Ndondo Cup 2017 kati ya Misosi FC dhidi ya Keko Furniture imeweka rekodi baada ya kushuhudia penati nyingi kwenye mchezo mmoja wakati wa kutafuta mshindi wa mechi hiyo atakaefuzu kucheza fainali.

Mchezo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, kwa mujibu wa kanuni za mashindano timu huelekea moja kwa moja kwenye matuta ili kupata mshindi atakaesonga mbele kwenye hatua inayofuata.

Misosi wakafanikiwa kushinda kwa penati 10-9 dhidi ya Keko Furniture ambayo imeka rekodi kwenye mashindano ya Ndondo kwa kuwa mechi ambayo imeamuliwa kwa mikwaju mingi ya penati. Jumla ya penati zilizopigwa ni 20 (Misosi 10 na Keko 10) penati 19 zimefungwa (Misosi 10, Keko 9) huku penati moja ikipaa juu (ya mchezaji wa Keko).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here