Home Kimataifa Coutinho kwenda Barca huku Chamberlain akienda Chelsea

Coutinho kwenda Barca huku Chamberlain akienda Chelsea

9194
0
SHARE

Baada ya Neymar kuwakimbia na kwenda PSG sasa inasemekana klabu ya Barcelona iko mbioni kukamilisha usajili wa Osmane Dembele kutoka BvB Phellipe Coutinho anayetoka Liverpool.

Klabu ya Chelsea wanaonekana wako serious sana na ishu ya kumnunua Oxlade Chamberlain, inasemekana mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wamejiandaa kutoa £25m kumnunua.

Baada ya usiku wa jana Real Madrid kumuanzisha Gareth Bale sasa kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kwamba haiwezekani tena kumnunua.

Klabu ya soka ya PSG inaonekana inataka kuonesha tena umwamba wake katika matumizi ya pesa na safari hii wamepiga hodi Atletico Madrid kumnunua mlinda lango Jan Oblak.

Klabu ya Chelsea imejiweka mkao wa kula baada ya kiungo wanayemtaka toka Leicester City Drinking Water kusema kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Inaonekana ka vita ya United na Chelsea katika usajili imerudi upya baada ya Chelsea nao kumtaka Serge Aurier ambaye hapo mwanzo Manchester United walikuwa wakimtaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here