Home Kitaifa Clouds 360 na Misosi yao hadi fainali Ndondo Cup 2017

Clouds 360 na Misosi yao hadi fainali Ndondo Cup 2017

3108
0
SHARE

Utatu wa Babbie Kabae, Sam Sasali na Hassani Ngoma wa clouds 360 umetoa kichapo kwa Adam Mchovu, Mamybaby, Kenedy The Remedy, DJ Sinyorita, DJ DOmmy na team nzima ya XXL baada ya ushindi wa Misosi FC uliowapeleka fainali dhidi ya Keko Furniture.

Ilikua ni mechi ya aina yake huku kila timu ikipewa nguvu na kipindi chake, Misosi FC chini ya Clouds 360 Hassan Ngoma aliungana na benchi la ufundi la timu yake kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Wazee wa XXL pia ambao wapo nyuma ya Keko Furniture walikuwepo uwanjani wakiongozwa na Dozen pamoja na Baba la baba Adam Mchomvu.

Dakika 90 zikakatika huku timu zote zikiwa hazijafungana ndipo mechi hiyo ya nusu fainali ya kwanza ya Ndondo Cup 2017 ikabidi iamuliwe kwa matuta. Hatua hii ilikuwa ni ya kuvutia sana kwani kila timu ilifanikiwa kufunga pebati zote tano za kwanza.

Zikaanza kupigwa penati moja moja, Misosi wakafunga penati nyingine mojamoja, Misosi wakafunga penati tano huku Keko Furniture wao wakifunga nne. Kwa hiyo Misosi wamesonga mbele kwa ushindi wa penati 10-9 dhidi ya Keko Furniture.

Misosi watacheza fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya nusu fainali kati ya Goms United na Kibada One ambao watacheza kesho Alhamisi August 10, 2017 kwenye uwanja wa Kenesi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here