Home Kimataifa Real Madrid waizamisha Manchester United

Real Madrid waizamisha Manchester United

5007
0
SHARE

Hii leo ndio mchezo wa fainali ya Super Cup kati ya mabingwa wa Champions league Real Madrid dhidi ya mabingwa wa Europa League klabu ya Manchester United.

Mtanange huu uliopigwa Telekom Arena ulikuwa unasubiriwa sana na wafuatiliaji wa masuala ya soka kutokana na ushindani baina ya miamba hii mikubwa ya soka duniani.

Real Madrid walianza kulichungulia lango la Manchester United dakika ya 24 kupitia kwa Casemiro ambapo bao hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili Real Madrid walioonekana kuliandama sana lango la Manchester United walipata bao la pili dakika ya 52 na safari hii alikuwa ni Isco aliyeitungua United.

Romelu Lukaku amezidi kuonesha kwamba amekuja Manchester United kwa kazi moja tu ya kufunga kwani katika dakika ya 62 aliipatia United bao la kufutia machozi.

Jumla ya thamani ya vikosi vyote viwili kwa jumla na waliokuwa benchi ni £913m, huku kikosi cha kwanza cha United kilichoanza thamani yake ni £377m huku kikosi cha Real Madrid kilichoanza kikiwa na thamani ya £247m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here