Home Kimataifa Real Madrid vs Manchester United nani kuibuka kidedea?

Real Madrid vs Manchester United nani kuibuka kidedea?

4121
0
SHARE

Leo ndio leo ambapo mabingwa wa Europa League Manchester United watapambana dhidi ya mabingwa wa Champions League klabu ya Real Madrid.

Hapo mwanzo kulikuwa na tetesi kwamba Cristiano Ronaldo atakosa mchezo huu bada ya kuchelewa kuanza mazoezi lakini hapo jana Real Madrid walimtangaza kuwepo katika kikosi.

Real Madrid ambao katika fainali mbili za mwisho za Champions League wamechukua zote wanaingia kupambana na United ambao wiki chache zilizopita waliwafunga katika mchezo wa kirafiki nchini Marekani.

Fainali ya leo ni muhimu sana kwa kiungo Michael Carrick ambaye kama akishinda mchezo huu baasi atakuwa ameshinda medali zote katika ngazi ya vilabu.

Real Madrid wataingia kifua mbele kwa kujiamini kwani rekodi inaonesha kwamba katika michezo mitatu ya mwisho ya Super Cup Madrid walishinda michezo yote.

Real Madrid wanaonekana wababe sana kwa timu za Uingereza na wameshakutana na United mara 11 wakishinda michezo 4 huku wakifungwa 2 na iliyobaki ikawa suluhu.

Hii leo Madrid watakuwa na kikosi chao kilekile kilichobeba Champions League huku United wakiwa na maingizo mapya Romelu Lukaku, Nemanja Matic na Victor Lindelof.

Kama zilivyo fainali nyingine, hii nayo inaweza kuwa fainali ngumu sana ukizingatia kwamba pande zote mbili zinaonekana kuwa katika kiwango kizuri sana siku za usoni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here