Home Kimataifa Barcelona wazidi kumng’ang’ania Phellipe Coutinho

Barcelona wazidi kumng’ang’ania Phellipe Coutinho

4413
0
SHARE

Klabu ya Barcelona wanaonekana hawataki kuelewa kauli za Jurgen Klopp kwamba Phellipe Coutinho hauzwi na hakuna dau lolote linaloweza kumng’oa kutoka Anfield, baada ya dau la kwanza la euro 80m kukataliwa sasa Barca wanaenda kuongeza 20 zingine kumnasa Coutinho.

Habari nyingine za usajili ni kwamba baada ya Manchester United kumkosa Eric Dier sasa klabu ya Bayern Munich inajiandaa kuwajaribu Tottenham Hotspur kwa kumnunua kiungo huyo huku wakiwa na kiasi cha euro 55m katika begi lao.

Katika kuendelea kuhakikisha kwamba wanarudisha heshima ndani ya klabu yao, Ac Millan wanajipanga kumrudisha Zlatan Ibrahimovich huku wakala wake Massimo Mirabelli akikiri uwezekano wa kutikea jambo hilo.

Baada ya tetesi nyingi sana kuhusu kuondoka kwake sasa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez anaonekana kukubali kubaki katika klabu yake ya Arsenal huku akiangalia mustakabali wa maisha mengine ndani ya klabu hiyo.

Baada ya kipigo kutoka Arsenal katika mchezo wa ngao ya hisani sasa kocha wa Chelsea Antonio Conte anataka kusajili wachezaji wengine huku jina la mlinzi Virgil Van Dijik likiongoza orodha ya wachezaji wanaohitajika darajani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here