Home Kimataifa Barcelona wamaliza hasira za kuondoka Neymar kwa Chapecoense

Barcelona wamaliza hasira za kuondoka Neymar kwa Chapecoense

6225
0
SHARE

Baada ya tukio la ajali ya ndege lililopoteza 90% ya timu yao mwaka jana, hii leo klabu ya Chapecoense iliikaribisha Barcelona waliotoka kumpoteza mshambuliaji wao Neymar Dos Santos.

Barcelona waliibamiza bila huruma Chapecoense mabao matano kwa sifuri, alianza Gerard Deulofeue kuifungulia Barca ukurasa wa mabao kabla ya Sergio Bosquet kuongeza bao la pili.

Lioneil Messi dakika ya 28 aliiandikia Barcelona bao la tatu na hivyo kwenda mapumzikoni vijana hao wa Nou Camp wakiongoza kwa bao tatu kwa sifuri.

Dakika ya 55 Luis Suarez aliendelea kuisulubu Chapecoense kwa kuiandikia bao la nne, na Dennis Suarez dakika ya 74 alikamilisha sherehe ya mabao kwa Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here